Img 20220803 Wa0032
Menejimenti na uongozi wa bodi ya chama cha Ushirika wa akiba na mikopo cha walimu Moshi Vijijini (Moshi Rural Teacher's Saccos Ltd) wanawatangazia wanachama wake wote kuwa mkutano Mkuu wa (25) Utafanyika kitarafa kuanzia tarehe 9.12.2022 hadi 13.12.2022 kuanzia saaa 2.00 asubuhi. Aidha uongozi huo umetoa angalizo kua wanachama wote wanahimizwa kuwahi na kushiriki vyema. Milango ya kujiandiksha itafungwa saa 3.00 asubuhi.
Kadhalika kila mwanachama afike na kitambulisho au hati ya umiliki wa hisa na atakaefika baada ya saa 3.00 asubuhi hatasajiliwa. HAIRUHUSIWI KUMWAKILISHA MWANACHAMA KWENYE MKUTANO. Pia wametoa chapisho la kitabu cha mkutano huo mkuu wa 25 likiwa na Dondoo wa mkutano mkuu pamoja na agenda nyingine mbalimbali. Unaweza kupakua (Download) hapa chini.