SEMINA NA MAFUNZO KWA WANACHAMA WA MRT SACCOS 2022

Img 20220803 Wa0035

Moshi Rural Teacher's Saccos (MRT SACCOS Ltd) ambacho ni chama mwanachama wa SCCULT (1992) Ltd imeendeleza msingi wa tano wa ushirika wa Elimu, Mafunzo na Taarifa.

Chama hiki kimefanya mafunzo kwa wanachama wake kwa siku tano na kuwafikia wanachama wake zaidi ya 2500 kwa tarafa nne ndani ya siku tano.Mafunzo hayo yalianza tarehe 01/08/2022 na yalifunguliwa rasmi na mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mh. Abbas Kayanda ambapo aliwakabidhi vyeti vya pongezi kwa wastaafu wote walioshiriki.

Pia Mrajisi msaidizi wa mkoa wa Kilimanjaro Bi. Jacqueline Senzighe ameshiriki mafunzo hayo na kusisitiza wanachama kufanyia kazi wanayojifunza ili kuzidi kuboresha chama chao na zaidi kutumia huduma za chama chao.

Siku ya tarehe 01/8/2022 walimu wastaafu ambao ni wanachama wamepatiwa mafunzo hayo yakigusa maisha yao baada ya kustaafu na kufurahia manufaa wanayoyapata kutoka kwenye chama chao hasa mafunzo na semina za mara kwa mara kupitia watoa mada wabobezi.

Pia siku ya tarehe 02.08.2022 Wanachama kutoka Tarafa ya Hai Mashariki wamepatiwa mafunzo ya wanachama.

Pia siku 03.08.2022 wanachama wa Tarafa ya kibosho wamefurahia mafunzo hayo na kuendelea kuweka imani kubwa na chama chao.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hotel ya YMCA Moshi mjini.Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Kilacha Social Hall.

Mada ambazo zimepamba mafunzo hayo ni pamoja na 

  1. Maisha kabla na baada ya kustaafu

  2. Mwalimu na ujasiriamali

  3. Uwekezaji na usimamizi wa rasilimali

  4. Umuhimu wa kutumia bidhaa na huduma za MRT SACCOS.

Sambamba na mafunzo hayo kumekuwa na uhamasishaji wa kushiriki kwenye sensa za watu na makazi kwa maendeleo ya Taifa itakayofanyika tarehe 23.08.2022 nchi nzima.

Huu umekua utaratibu kwa chama cha walimu Moshi vijijini  kuwafikia wanachama wake kwa njia mbalimbali kama  mafunzo na huduma bora kidigitali.

Download File/s: